Dimba la dunia la wanawake kuanza Canada
Michuano ya kombe la dunia la wanawake inatarajiwa kuanza baadaye hii
leo nchini Canada, ikiwa ni michuano ya kwanza mikubwa ya kandanda
kufanyika tangu shirikisho la soka FIFA kukumbwa na upepo mbaya wa
kashfa ya rushwa.
Hii ndio michuano mikubwa zaidi kwa soka la
wanawake duniani, zaidi ya watu bilioni moja wanatarajiwa kushuhudia
michuano hiyo kwa njia ya televisheni.Mechi ya ufunguzi itakuwa baina ya wenyeji Canada dhidi ya China.
Timu za Ujerumani, Marekani na Ufaransa zinapewa nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo.
Waandalizi wa michuano hiyo wamekataa matatizo ya FIFA kuwachanganya kwenye shughuli za uaandaaji wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment