Sheria ya ndoa za jinsia moja yaanzishwa
Kinara
mkuu wa chama cha upinzani cha Labour nchini Australia, ameanzisha
sheria inayokubalia ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo
inapingwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi huyo,
Bill Shorten, amemtaka Abbott kuwakubalia wanachama wa serikali
wawe na uhuru wa kupiga kura kuhusiana na swala hilo.Abbot ambaye ni mfuasi wa kanisa katoliki alikataa kura ya uhuru wa ndoa za jinsia moja na kusema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.
No comments:
Post a Comment