Monday, June 1, 2015

MWANAMKE WA KUIGWA

 Mkazi wa kijiji cha Jirihini  kata ya Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, Mwanakombo Said, akisonga ugali na kuwauzia wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)  eneo la Mbugani kunakofanyika  utafiti wa awali na  kuonyesha   uwepo wa mafuta na gesi umbali wa zaidi ya  kilometa 10 kutoka kijiji cha Jirihini.
Tangakumekuchablog
Mkinga
MWANAKOMBO amewataka wanawake wenzake waache kujikalia vibarazani na kuunda umbea pamoja na kuwategemea wanaume zao au mabwana  na badala yake watafute njia za kujipatia pesa kwa njia za halali.
Alisema haikuwa rahisi kwake kuweza kujitoa mhanga na kuwafuata wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji Madini kupika na kuwauzia chakula ambapo kwa siku amekuwa akipata zaidi ya shilingi laki moja tokea asubuhi.
Alisema eneo hilo limekuwa likitembelewa na watu mbalimbali kujionea namna ya hatua za Uchorongaji huo unaofanywa na Kampuni ya  Madini ya STAMICO.
Alisema amekuwa kitoka alfajiri nyumbani kwake kwa kukodi pikipiki (bodaboda) kupakiza maji, na vyombo vyengine vya kutayarishia chai na chakula ambao mwanzo watu wengi walikuwa wanambeza na kuonekana kujihangaisha.
Alisema kwa sasa amekuwa akivuna pesa na mara baada ya mradi huo kukamilika atakuwa na mtaji wa kufungua biashara au saloon ya kisasa na hivyo kuwataka wanawake wenzake kujituma kwani fursa nyingi za kujipatia kipato kwa nia za halali zipo.





No comments:

Post a Comment