Uchambuzi huu wa magazeti unaltwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
MWANANCHI
Mwenyekiti wa CCM, Simiyu Musa Ntimizi amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti kijana mmoja mkazi wa Manispaa ya Tabora.
Mwenyekiti huyo alisomewa mashtaka mbele
ya hakimu na kudaiwa kufanya koda hilo nyumbani kwake kwa kumrubuni
kijana huyo kwa kumnunulia bia mbili kwenye baa moja mjini Tabora kabla
ya kutenda kosa hilo.
Wakili Jocktan Rusherwa alidai kuwa
baada ya kijana huyo kulewa na kupoteza fahamu, mshtakiwa alimpeleka
nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo mshtakiwa alikana tuhuma hizo na yupo nje kwa dhamana na wakili kuahirisha kesi hiyo hadi itakaposomwa tena kesho.
MWANANCHI
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
ametangaza nia yake ya kugombea urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba akieleza jinsi atakavyoivusha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi
wa kati utakaopatikana kwa kutoa haki kwa watu wote.
Akitangaza nia hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Mipango Dodoma, Nchemba alisema: “Ahadi
yangu kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha. Nitawavusha wanaCCM wenzangu
pamoja na Watanzania kwa ujumla… wakati ni sasa tunataka Taifa letu
lifike kuwa nchi yenye uchumi wa kati,” alisema Nchemba na kuongeza:
“Ninachoomba
kutoka kwenu, mniamini na mniunge mkono katika hili… nitawavusha.
Lakini tukumbuke kwamba kila mmoja lazima atimize wajibu wake katika
utendaji kazi ili tufikie huko tunapotaka kufikia.”
Nchemba aliyekuwa ameongozana na mkewe, Neema na watoto wake watatu, Isaack, Grecious na Joshua
pamoja na ndugu jamaa na marafiki, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo
hayo, lazima nchi iwe na mfumo wa uwajibikaji utakaowezesha kulinda
rasilimali za Taifa na kuongeza Pato la Taifa.
Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko ni Matendo, Wakati ni Sasa’,
ambayo ataitumia katika safari yake ya kuelekea Ikulu, Nchemba
aliyetumia dakika 115, kuanzia saa 10.10 jioni hadi saa 11.25 jioni,
alisema atapambana na tabia za watu kufanya kazi kwa mazoea, rushwa,
ufisadi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano atakayoiongoza endapo
atachaguliwa, itakuwa ya uadilifu na uaminifu.
Alisema iwapo atachaguliwa, ataifanya
nchi kuwa ya kipato cha kati sambamba na watu wake, kujenga Taifa
linalojitegemea kibajeti na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi
wao wenyewe.
Jambo la kwanza na la msingi ni kuitambua ajenda ya Watanzania, Watanzania watamuunga mkono kiongozi kwa kuitambua ajenda yake,” alisema.
Alisema wakati akijitathimini kutangaza
nia ya kugombea alikuwa akifahamu ajenda ya Watanzania, huku akisisitiza
kuwa umaskini hakuusoma katika vitabu, bali amekulia katika maisha ya
kimaskini.
NIPASHE
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameishauri serikali ya Burundi kusogeza mbele mwezi mmoja na nusu uchaguzi mkuu nchini humo.
Uchaguzi wa wabunge ulitarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii na wa urais ukipangwa kufanyika mwezi huu.
Hatua hiyo imetokana na kutoimarika kwa
hali ya amani na utulivu kufuatia baadhi ya vyama vya upinzani na
mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea na maandamano kupinga hatua ya
Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza, kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Taarifa ya kuomba kusogezwa mbele kwa
uchaguzi huo ilitolewa jana na wakuu wa nchi hizo katika mkutano wao
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibela, alisema wakuu hao waliishauri serikali ya Burundi kusogeza uchaguzi huo kutokana na nchi hiyo kutotengemaa kisiasa.
Alisema wakuu hao pia walitoa wito kwa
makundi yenye silaha kuziweka chini. Pia, waliishauri serikali ya
Burundi kuwarejesha raia wake wote waliokimbilia nchi jirani.
Dk. Sezibera alisema wakuu wa EAC pia
walitoa wito kwa wadau wa amani ukiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja
wa Afrika (AU), kuingilia kati mgogoro huo.
Waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa AEC, Rais Jakaya Kikwete (Tanzania); Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta; Rais wa Uganda, Yoweri Museveni huku Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akihudhuria kama mlezi wa Burundi.
Rwanda iliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Valentine Rugwaiza huku Burundi ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Allen Nyamizwe.
NIPASHE
Shirika lisilo la Kiserikali la Sikika
limewaasa wabunge kuishinikiza serikali iongeze bajeti ya dawa muhimu na
vifaa tiba kwa mwaka 2015/16, ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa
nchini unaongezeka kufikia asilimia 80, kama inavyotarajiwa na mpango
wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Aidha, imewataka waishinikize itoe fedha
zote zinazoidhinishwa na Bunge kwa wakati, ili kuviwezesha vituo vya
huduma za afya vya umma kuondokana na uhaba wa mara kwa mara wa dawa
muhimu na vifaa vya tiba, na hivyo kuimarisha afya za wananchi walio
wengi.
Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi wa Sikika, Irenei Kiria (pichani) na kuongeza kuwa
wabunge wanapaswa kulichukulia suala hili kwa umuhimu wa kipekee na
kuachana na itikadi za vyama, ili kuokoa maisha ya Watanzania, hasa
wanaotegemea kupata matibabu katika vituo vya huduma za afya vya umma
nchini.
“Ukiangalia
bajeti iliyotengwa kwa ajili ya dawa muhimu na vifaa tiba kwa mwaka wa
fedha wa mwaka 2015/16, kwenye bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii inayosomwa kesho, ni Shilingi bilioni 37 tu kati ya mahitaji
halisi ya zaidi ya Shilingi bilioni 500, fedha ambazo ni kidogo sana,” alisema.
Alisema bajeti hiyo imepungua kwa
kiwango kikubwa ukilinganisha na bajeti ya miaka ya nyuma kwa mfano
kuanzia mwaka 2011/12, kuonyesha namna serikali isivyotoa kipaumbele kwa
eneo hilo lililo muhimu kwa ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kiria alisema mwaka 2011/12, mahitaji
halisi ya bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba yalikuwa Sh. bilioni 188,
lakini jumla ya bajeti iliyopitishwa ilikuwa Sh. bilioni 123.4, na
serikali ikatoa Sh. bilioni 98 (79.4%) ya fedha iliyoidhinishwa.
Alisema mwaka 2012/13 mahitaji halisi ya
fedha kwenye eneo hilo yalikuwa Sh. bilioni 198, lakini bajeti
iliyopitishwa ilikuwa Sh. bilioni 80.5 na serikali ikatoa fedha zote
hizo.
“Japo
tatizo likabaki kuwa ni fedha kuchelewa kutolewa kwa wakati na hivyo
kuzorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa upatikanaji
wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya huduma za afya vya umma,
ni moja ya viashiria vya huduma bora za afya katika nchi yoyote ile,” alisema.
Aidha alisema mwaka 2013/14, mahitaji
halisi ya fedha yalikuwa Sh. bilioni 549, lakini bajeti iliyoidhinishwa
ilikuwa Sh. bilioni 64, na serikali ikatoa Sh. bilioni 50 (78.9%).
Kwa mujibu wa Kiria, mahitaji halisi ya
fedha kwa mwaka 2014/15, yalikuwa Sh. bilioni 577, lakini fedha
iliyoidhinishwa ilikuwa Sh. bilioni 70.5, na fedha iliyotolewa hadi sasa
ni Sh. bilioni 23.5.
NIPASHE
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),
imesema ilichelewa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini
kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuchelewa kwa fedha kutoka
serikalini, marejesho madogo ya mikopo na uchache wa fedha
zilizokusanywa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa,
alisema HESLB ilishindwa kupeleka fedha kwa wakati kutokana na vyanzo
vilivyotegemewa kutoa fedha kuchelewesha huku akisisitiza kuwa fedha
iliyokwisha kusanywa haikuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi wenye
mahitaji.
“Siyo
kama inavyoelezwa na vyombo vya habari, mikopo katika mihula yote ya
kwanza ilitolewa kwa wakati, katika kipindi hiki cha muhula wa mwisho wa
masomo mikopo imechelewa kwa sababu ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya
mikopo kuchelewa na urudishaji wa mikopo usioridhisha, Mwaisobwa.
Aidha, alisema mikopo haikuchelewa
kupelekwa katika vyuo vyote vyenye wanafunzi wenye mahitaji na kuongeza
kuwa hata vyuo vilivyofanya migomo, baadhi ya vitivo vilikuwa vimepatiwa
mikopo.
Alisisitiza kuwa HESLB imeshapeleka
fedha za mikopo kwenye vyuo vyote na kuwa vyuo ambavyo wanafunzi
hawajapokea, vina utaratibu wake wa kuwapatia fedha hizo.
Hivi karibuni, wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini vikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Iringa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu cha Dar es Salaam (DUCE) waligomea masomo kuishinikiza serikali kupitia HESLB kuwapatia fedha za kujikimu.
NIPASHE
Serikali imeombwa kuangalia upya tatizo
la ukubwa wa kodi kwa hospitali binafsi kwani lengo kuu ni kutoa hudumu
bora kwa gharama nafuu kwa kila Mtanzania.
Ombi hilo lilitolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam (RMC), Dk. Amish Kanabar, wakati wa ujio wa Mwenge wa Uhuru kwenye hospitali hiyo ambao ulizindua jengo jipya la ghorofa 10 la hospitali hiyo.
Alisema hospitali binafsi na za serikali
zina lengo la kuwahudumia Watanzania kupata afya bora, hivyo hakuna
haja ya kutoza kodi kubwa kwani hali hiyo inazidumaza na kushindwa kukua
kwa kasi.
Alisema katika kuhakikisha wanaendelea
kutoa huduma bora, RMC imechukua mkopo ghali kutoka benki na hata kuweka
rehani hisa za wanachama wake ili kufanikisha ujenzi wa jengo jipya.
“RMC
inafanya jitihada kuhakikisha inakuwa chuo cha mafunzo ya uuguzi na
utaalam wa tiba na afya ili kupunguza pengo la nguvu kazi katika sekta
ya afya Tanzania. Mara zote RMC imekuwa ikishirikiana na sekta ya umma,
Manispaa ya Ilala na Lions Club ya Dar es Salaam Host na Shirika La
Nyumba La Taifa, “ alisema.
Alisema hospitali inatoa huduma kwa
wastani wa wagonjwa 500 kwa siku na kwamba upanuzi wa jengo una maslahi
mapana kitaifa kama vile kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa
gharama nafuu, kutekeleza kwa vitendo sera za Mkukuta II na Dira ya
Taifa 2025 na kuongeza wigo wa ajira na mafunzo kwenye sekta ya afya
Tanzania
MTANZANIA
Utangazaji nia ya kuwania urais kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kwa kishindo, huku machifu wote wa
Mkoa wa Mbeya wakitarajiwa kumuunga mkono Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Prof. Mark Mwandosya, ambaye leo anatarajiwa kutangaza nia mkoani Mbeya.
Miongoni mwao ni Chifu wa Rungwe, Mbozi na Chifu wa Jiji la Mbeya, Mwashiga ambaye atawaongoza pia wazee wote wa jiji hilo.
Wakati hayo yakijiri, wakazi wa Jiji la
Mbeya wakiwamo vijana, pia wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi
kumsindikiza Profesa Mwandosya kutangaza nia.
Hafla hiyo inayotarajiwa kufanyika saa
nne asubuhi, itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo eneo
la Soko Matola jijini Mbeya.
Katika hafla hiyo, viongozi wa vyama
mbalimbali vya siasa vilivyo nje ya Ukawa wanatarajiwa kuhudhuria ikiwa
ni pamoja na kupata nafasi ya kutoa msimamo wao wa kumuunga mkono
Profesa Mwandosya.
Vyama hivyo ni TLP, ACT-Wazalendo, APPT- Maendeleo, UDP, PP, SAU na UPDP.
Wakati Mwandosya akiwa Mbeya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere naye anatarajia kutangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama.
Wakati hayo yakijiri, Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja pamoja na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani wao wakitarajiwa kutangaza kesho jijini Mwanza.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
amesema siku saba zijazo kuanzia sasa atachukua fomu ya kuomba
kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea urais wa Tanzania.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Arusha
baada ya kumalizika ibada ya kwanza aliyoshiriki katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati,
Usharika wa Arusha mjini.
“Nimekuja
kanisani kuabudu, nimefarijika kwa neno la Mungu. Nataka kusema,
nilishatangaza nia miezi saba iliyopita, Desemba mwaka jana,” Nyalandu
Kwa upande waje Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema atatangaza nia ya kuwania urais Juni 6, mwaka huu jimboni kwake Mtama mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment