Ukivuta sigara hadharani China kuna faini zake!!
China iliwahi kupitisha sheria ya
kusitisha uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya
shule na hospitali lakini haikuweza kutekelezeka kwa mara ya kwanza.
Ingawa kuna baadhi ya nchi kama Jamaica
ambapo uvutaji sigara ama bangi si kitu cha ajabu lakini kwa upande wa
China sasa kitendo hicho kimeonekana ni kosa kubwa na Serikali imeanza
mikakati ya kuhakikisha inatokomeza uvutaji sigara.
Nchi hiyo imerudi kwenye headlines tena
na safari hii Serikali imeweka wazi mikakati yake hiyo ya kuzuia uvutaji
wa sigara kuanza leo katika maeneo ya wazi hasa ya mji mkuu wa nchini
hiyo Beijing na kinyume na hapo kuna faini ambazo zitatolewa kwa
wanaokaidi agizo hilo.
Ripoti ya Wizara ya afya imesema nchi hiyo ina wavutaji wa sigara zaidi ya milioni 300,
Sheria hiyo imesema watakaoukiuka
makubaliano hayo watatozwa faini ya fedha ya China yuan 32.25 ambayo ni
sawa na dola 1.60 huku watakaorudia kosa hilo kwa zaidi ya mara tatu
watatozwa faini ya dola 1600 pamoja na kuwekwa kwenye website ya
Serikali.
Pia Serikali imetoa onyo kwa wauzaji wa
sigara kuhakikisha wanauza kuanzia mita 100 kutoka katika ameneo ya wazi
na karibu na shule ama hospitali ili kukwepa faini hizo.Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika usiwe mbali nami, ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment