Tuesday, June 16, 2015

VIWANJA 10 VILIVYO MBALI NA MJI DUNIANI

Picha za Viwanja 10 vya ndege vilivyo mbali zaidi na Miji Duniani..

Uwanja wa Ndege
Mara nyingi inasikika ndani ya vikao vya Bunge kuhusu ishu ya jinsi kuwahamisha watu wanaoishi pembeni ya Viwanja vya ndege ili Viwanja vitanuliwe.. kuna waliofuata Viwanja na kuanzisha makazi yao, ishu ni Kiwanja kiondoke kwenda mbali au watu waondolewe viwanja vitanuliwe?
Nimekutana na hii ripoti ya Daily Mail iliyotolewa June 04 2015.. inaonesha Viwanja vya Ndege vilivyojengwa mbali zaidi na Miji.
.
Paris Vatry Airport.. Uwanja uko umbali wa kama Kilometa 210 toka Jiji la Paris, Ufaransa.
Oslo-Torp Airport
Oslo-Torp Airport.. Huu uwanja uko umbali wa Kilometa 117 kutoka Oslo ambapo ni Mji Mkuu wa Norway. Ukitaka kufika Town inabidi utumie taxi au usafiri wa treni.
Munich West Airport
Munich West Airport. Ukisikia jina la huu Uwanja unaweza kuhisi kwamba uko ndani ya Mji Mkuu wa Ujerumani, Munich. Lakini ukweli ni kwamba Uwanja huu wa ndege uko Memmingen. Na bado Umbali wa kutoka Uwanjani mpaka kwenye Mji ni Kilometa 112.
Frankfurt (Hahn)
Frankfurt (Hahn). Uwanja huu wa Ndege uko umbali wa kama kilometa 109 kutoka Mji wa Frankfurt, Ujerumani.
.
London Oxford Airport, uwanja uko umbali wa Kilometa 98 kutoka katikati ya Jiji la London.
Stokholm
Stockholm Skavsta Airport. Kutoka hapo mpaka ufike Stockholm Town, Sweden ni umbali wa Kilometa 97
.
Barcelona Girona Airport, uwanja ulipo na katikati ya Jiji la Barcelona ni umbali wa Kilometa 93.
.
Barcelona Reus Airport.. Hapa napo umbali wake mpaka kufika Barcelona town ni Kilometa 93 mtu wangu.
.
Paris Vatry Airport, kutoka hapa mpaka ufike katikati ya Paris, Ufaransa ni Kilometa 86.
.-
Ndani ya Ujerumani mtu wangu, hapa ni Dusseldorf Airport.. Kutoka hapa mpaka kufika katikati ya Jiji la Dusseldorf ni Kilometa 49 pia.

No comments:

Post a Comment