Mlima Everest ulisonga kufuatia tetemeko
Watafiti
wa maswala ya ardhi kutoka China wanasema kuwa mlima Everest
ulisogea takriban sentimita tatu kufuatia tetemeko kubwa la ardhi
lililotikisa Nepal mwezi Aprili.
Hata hivyo watafiti hao wanasema kuwa mlima huo ungali kimo hicho hicho.Takriban watu elfu nane waliangamia tetemeko hilo lililofika kipimo cha 7.8 kwenye mizani ya Richter lilipokumba eneo la mlima Everest.
Tetemeko hilo lilisababisha maporomoko ya ardhi na theluji kutoka mlima huo mrefu zaidi duniani.
Ajabu ni kuwa sasa wanasayansi nchini Nepal na wanasema kuwa mji mkuu wa Kathmandu umesogea kwa zaidi ya mita mbili kuelekea Kusini.
No comments:
Post a Comment