Waandamana wakiwa uchi Uganda
Wanawake
katika kijiji kimoja cha kaskazini mwa Uganda wamefanya maandamano
wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na
jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10.
Wakati wa
maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata
kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake
No comments:
Post a Comment