Wilshere:Mimi ni Arsenal sitaki Man City
Kiungo
cha kati wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Jack Wilshere amekaririwa na kusema kuwa nia yake ni kusalia Emeirate licha ya dukuduku kuwa wapinzani wao wakuu klabu
ya Manchester City wanakamia kumsajili msimu ujao.
City
waliomaliza katika nafasi ya pili msimu huu wako mbioni kuratibu
mabadiliko ya vipengele vya kanuni ya shirikisho la soka nchini Uingereza
itakayohitaji vilabu kuimarisha idadi ya wachezaji wa asili ya
Uingereza.Yamkini klabu hiyo tajiri haina budi kuwasajili wachezaji zaidi ya wawili baada ya kuondoka kwa James Milner na Frank Lampard.
Wilshere alishiriki mechi 9 pekee msimu uliopita baada ya kujeruhiwa mguu na kulazimika kukaa nje kwa takriban miezi 6.
Kiungo huyo anasema ndoto yake kuu ni kuiga mfano wa mchezaji bora duniani Lionel Messi na
Andres Iniesta ambao baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu na kukosa makali walijifurukuta na kuibuka kuwa viungo dhabiti wa klabu bingwa barani Ulaya na Uhispania Barcelona.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alinukuliwa akisema kuwa mchezaji huyo anahitaji takriban misimu miwili ilikupona kabisa jeraha lake linalomsumbua sana la kifundo cha mguu.
No comments:
Post a Comment