Shirika la ndege taabani kwa kupakua mjusi
Magazeti nchini India yameripoti Leo kisa cha kutamanisha kilichotokea katika ndege ya shirika la Air India.
Abiria
mmoja aliyekuwa safarini kuelekea mjini London Uingereza akitumia ndege
ya shirika la ndege ya Air India alizua hofu miongoni mwa abiria
wengine alipopiga kelele na kupata mshtuko baada ya kumpata mjusi kafiri ndani
ya mlo wake.Abiria wote walitaharuki wasijue kilichompata mwenzao hasa wakati huo ambapo kunataharuki kubwa na tahadhari kuhusiana na maswala ya usalama kufuatia matukio ya Kigaidi duniani.
Mjusi kwenye mkate
Abiria huyo ambaye awali alikuwa ameagiza chakula maalum kutoka kwa mhudumu wa ndege hakuamini macho yake alipokaribia kumla mjusi macho makavu !
Inasemekana kuwa alipofungua mkate wake akitaka kuunga'ta mara akaona ukitikisika .
Ghafla na kaona mjusi akijifurukuta akitafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye plastiki iliyokuwa imefunika chakula chake.
Shirika hilo limekanusha habari hiyo japo kuna picha inayoendelea kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikionesha mjusi mdogo kwenye mkate .
Waziri wa usafiri wa anga ametao onyo kwa shirika hilo akisema kuwa halifai kuwapakulia wateja wake mijusi !
Maoni yako
Ungefanyaje wewe ?
Usiache kuniandikia maoni yako kupitia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment