Arsenal yakubali kipigo cha nne msimu huu dhidi ya Southampton,
Baada ya michezo tisa ya Ligi Kuu Uingereza kupigwa Jumamosi ya December 26 siku ya Boxing Day,
ulibakia mchezo mmoja ambao ulikuwa unachezwa usiku wa December 26.
Mchezo ambao ulikuwa unachezwa usiku wa December 26 ni mechi kati ya Southampton dhidi ya Arsenal katika dimba la St Mary’s lenye uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki 30000.
Huu ni mchezo ambao ulikuwa unatoa nafasi kwa Arsenal kukaa kileleni mwa Ligi Kuu kama ingefanikiwa kupata ushindi, kwa Leicester City wanaongoza Ligi hiyo wamekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Liverpool. Hivyo kama Arsenal wangefanikiwa kuifunga Southampton basi wangekuwa mbele ya Leicester City kwa tofauti ya point moja.
Dimba la St Mary’s limeonekana kuwa gumu kwa Arsenal kwa imeshindwa kutoa hata sare na kujiwesha kuondoka na point moja, kwani Arsenal ilikubali kipigo cha goli 4-0 dhidi ya Southampton. Magoli ya Southampton yalifungwa na Cuco Martina dakika ya 19, Shane Long dakika ya 55 na 90 na Jose Miguel Fonte dakika ya 69. Hii ni mechi ya 4 kufungwa kwa Arsenal katika jumla ya mechi zake 18 ilizocheza msimu huu.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa December 26
No comments:
Post a Comment