Saturday, December 26, 2015

VAN GAAL AELEA KIKAANGONI OLD TRAFORD

Kwa kipigo cha Stoke City, huenda siku za Van Gaal Man United zikawa zinahesabika …

Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena leo December 26 siku ya Boxing Day kwa michezo 10 ila mchezo wa awali ulikuwa kati ya Stoke City dhidi ya Manchester United katika dimba la Britannia lenye uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki 27000 kwa mara moja. Huu ni mchezo wa 18 kwa timu zote mbili ila unatajwa kuwa mgumu kwa Man United.
3500
Ugumu wa mchezo unatajwa ni kutokana na kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal kuhusishwa kufukuzwa kama timu itaendelea kufanya vibaya, hususani katika mchezo huo. Stori kutoka katika mitandao mingi ya Ulaya inaripoti kuwa Louis van Gaal atafukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho kitu ambacho kinaonekana kumuumiza kichwa Louis van Gaal.
3392
Dimba la Britannia lilikuwa gumu kwa Man United kwani waliamulia kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa wenyeji wao Stoke City, hali ilianza kuwa mbaya kwa Man United kuanzia dakika ya 19 baada ya Stoke City kupata goli la uongozi kupitia kwa Bojan Krkic na dakika ya 26 Marko Arnautovic akapachika goli la pila na la mwisho. Kwa matokeo hayo Louis van Gaal anazidi kuwa na hali mbaya ya kuendelea kusalia Man United.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog


No comments:

Post a Comment