Sunday, December 20, 2015

VAN GAAL NAE AKALIA KUTI KAVU

Sababu nne za kwa nini Man United wanatakiwa wamfukuze Louis van Gaal na kumuajiri Jose Mourinho …


Hizi ni stori au mkusanyiko wa mawazo ya waandishi wa habari wa Uingereza na wchambuzi wa masuala ya soka Uingereza, Jose Mourinho na Louis van Gaal ndio makocha ambao walikuwa wanahusishwa kwa kiasi kikubwa kupewa nafasi ya kufukuzwa kazi kutokana na mwenendo wa timu zao. Tayari Jose Mourinho kafukuzwa Chelsea ila hatujui Man United wataamua nini kwa Van Gaal. Hizi ndio zinatajwa kuwa sababu nne za Man United kumfukuza Van Gaal na kumuajiri Mourinho.
4- Ameifanya Man United kucheza mpira wa kuboa katika historia ya klabu hiyo.
Kama wewe ni shabiki wa Man United au la lakini ni ngumu kumuele kocha anayetumia pound milioni 250 kwa usajili halafu timu inacheza soka la kujilinda zaidi.
Uniteds-defence
3- Jose Mourinho ameshinda mataji mawili msimu uliopita lakini Louis van Gaal hajashinda kitu.
Inashangaza kuona kocha aliyetwaa matajai mawili msimu uliopita akiwa na Chelsea anafukuzwa kazi wakati kocha ambaye hajashinda taji lolote na kafanya usajili mkubwa amebakia na kuendelea kuifundisha Man United.
LONDON, ENGLAND - MARCH 01: Manager Jose Mourinho of Chelsea lies on the pitch as Chelsea celebrate with the trophy during the Capital One Cup Final match between Chelsea and Tottenham Hotspur at Wembley Stadium on March 1, 2015 in London, England. (Photo by Clive Rose/Getty Images)
2- Kuruhusu wachezaji 22 kuondoka Man Unite na aliowasajili hawajafanya kitu chochote cha maana.
Ni miezi 18 sasa toka Louis van Gaal ajiunge na Man United na tumeshuhudia wachezaji 22 wakiondoka Man United na kusajili wachezaji ambao bado hawajaifanyia Man United chochote cha maana. Van Gaal ameacha waondoke wachezaji kama Javier Hernandez na kujiunga na  Bayer Leverkusen, Hernandez akiwa na Bayer amefunga magoli 18 katika mechi 21.
Chichaz-copy
1- Van Gaal amefanya usajii wa pound milioni 250 lakini timu bado mbovu.
Usajili wa pound milioni 250 ulitarajia kuiona Man United ikicheza vizuri na kutwa mataji lakini mwisho wa siku imeishia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini hata mchezo au uwezo wa timu kimchezo katika mechi dhidi ya CSKA Moscow na PSV haikucheza mchezo mzuri kiasi hata cha beki wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand kuponda uwezo wa sasa wa klabu hiyo.
Louis-van-Gaal-anxietyKwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumechablog

No comments:

Post a Comment