Wednesday, December 16, 2015

FABREGAS APASUA JIPU

Fabregas kaongea haya kuhusu wachezaji wenzake wa Chelsea wanaolipwa mishahara mikubwa …

Klabu ya Chelsea ya Uingereza ni miongoni mwa vilabu vinavyolipa mishahara mikubwa wachezaji wake, klabu hiyo ambayo inamilikiwa na bilionea wa kirusi Roman Abromavich imekumbana na wakati mgumu msimu huu, baada ya kupokea jumla ya vipigo 9 katika mechi 16 ilizocheza.
Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho alinukuliwa siku moja nyuma akilaumu wachezaji wake wanamsaliti, ila December 16 kiungo wa kimataifa wa Hispania anayekipiga katika klabu ya Chelsea Cesc Fabregas amefunguka na kuwaambia wachezaji wenzake kuwa wanatakiwa kujituma na kucheza kwa juhudi kama ambavyo wanavyolipwa mishahara mikubwa.
cesc-fabregas-diego-costa-radamel-falcao-nemanja-matic-chelsea_3351169
“Kama wewe mchezaji staa na unalipwa mshahara mkubwa kama staa inabidi ucheze na kujituma kwa bidii kama mchezaji staa na anayelipwa mshahara mkubwa, kiukweli kuwa na msimu mbovu huwa inatokea ila inatakiwa ucheze kwa uwezo mkubwa hata kama itatokea umepoteza mchezo” >>> Fabregas
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment