Rais Magufuli hajaridhishwa mapambano ya rushwa, kaigeukia TAKUKURU
Bado Rais Magufuli anaendelea
kuipanga Serikali ya awamu ya tano ili kuhakikisha mambo yanakuwa sawa
kwenye utawala wake na kazi inakwenda. Tuhuma za rushwa na ubadhirifu
zimekuwa nyingi, baada ya ishu ya makontena bandarini, ukwepaji kodi
TRA, kaigeukia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko Taasisi ya TAKUKURU na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah ambapo kamteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola kukaimu nafasi hiyo.
Taarifa kutoka Ikulu hii hapa ambapo
ametangaza pia kuwasimamisha kazi watumishi wawili ambao walisafiri nje
ya nchi kinyume na maagizo yake.
No comments:
Post a Comment