Serikali: Tutalinda Haki za Binadamu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiingia katika ukumbi wa
Karimjee wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia wadau mbalimbali
hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani
yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipeana mkono na mhutimu wa Chuo
Kikuu Mzumbe mara baada ya kutoa burudani fupi wakati wa maadhimisho ya
Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea maandamano katika
Ukumbi wa Karimjee yaliyofanywa na wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu
wakati wa maadhimisho hayo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Kikosi cha Bendi ya Askari
magereza wakiongoza maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za
Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam
Kikosi cha Bendi ya Askari
magereza wakiongoza maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za
Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam
Wadau mbalimbali wakiwa katika
maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za Binadamu Duniani
yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa(UN) wakiwa na wadau mbalimbali katika maandamano ya kuadhimisha
siku ya Haki za Binadamu duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es
salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD – MAELEZO
……………………………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki _Maelezo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imesema itahakikisha Haki Za Binadamu zinalindwa na
kuheshimiwa na kila mtu katika jamii anayotoka bila kujali itikadi
yoyote ili kuleta usawa na uhuru katika jamii.
Akizungumza katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika katika ukumbi wa
Karimjee leo jijin Dar es Salaamu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesema atahakikisha anasimamia uhuru na haki kwa wananchi wote
kwakuwa binaadamu wote ni sawa na wote wana haki sawa.
Mhe Samia ameongeza kuwa Serikali
itahakikisha inakomesha mauaji ya albino,ukatili wa kijinsia hasa kwa
wanawake na wasichana, ndoa za utotoni,ukeketaji pamoja na mateso kwa
mahabusu kwa vile wote ni Binadamu na wana Haki sawa.
Aidha amesema kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba mbalimbali inayohusu Haki za
Binadamu kama vile Mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi wa mwaka
1965, Mkataba wa kuondoa Ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake wa
mwaka 1979 na Mkataba wa kimataifa wa haki za watoto wa mwaka 1989.
“Serikali yetu imekwisha ingiza
baadhi ya mikataba hii katika sharia zetu za nchi,ama kwa kuunda sharia
mpya au kurekebisha zile zilizopo”Alisema Mhe Samia.
Awali Mkurugenzi wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora Bw Bahame Tom Nyanduga katika hotuba yake
amesema kuwa Tume ya Haki za Binaadamu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kutoa elimu kuhusu haki za binaamu kwa wananchi wote japokua kuna
changamoto ndogo ndogo kwa maeneo ya vijijini na wanaendelea na jitihada
za kuwafikia wananchi hao.
“Haki na Wajibu ni vitu vinavyoambatana hivyo watu wote washiriki. “Alisema Bw Bahame.
Ameongeza kuwa ni lazima Haki za
Binaadamu zilindwe na kuheshimiwa ili kuleta maendeleo katika uchumi wa
jamii kwa ujumla kwa kuwa bila Uhuru na Haki watu watakosa elimu
bora,maji safi,uhuru wa kupata habari,kwa kuzingatia kuwa binadamu wote
wamezaliwa huru na ni sawa.
Maadhimisho hayo ni ya 67 tangu
yalipoanzishwa na Azimio la Ulimwengu la Haki za Binaadamu Mwaka 1948
yamehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Serikalini,Umoja wa
Mataifa,Wadau wa Haki za Biadamu, na wanachi kwa ujumla ambapo kauli
mbiu inasema “Haki Zetu,Uhuru Wetu Daima” .
Hata hivyo Tume ya Haki za
Binadamu imedhamiria kuleta maendeleo chanya kupitia Mpango wa Maendeleo
endelevu utakaonza januari mwakani ambao umekuja na malengo kumi na
saba ikiwemo elimu bora,afya bora, pamoja na kuondoa umaskini ili
kufikia malengo ya Millenia.
No comments:
Post a Comment