Christmas sio kila mtu anasherehekea, hawa hapa watakuwa kazini kama kawaida Uingereza..
December 25 huwa ni siku ambayo wakristo
wengi duniani wanaungana kwa pamoja kusherehekea sikukuu ya Christmas,
japo sikukuu inawahusu wakristo lakini huwa ni siku ya mapumziko kwa
ujumla kwa watu wote bila kujali dini zao.
Sasa nimekutana na hii stori kutoka
Uingereza, labda nikufahamishe tu kwamba kama ikitokea December 25 2015
utakuwa na jukumu au ratiba ya kazi usisononeke kwa sababu kuna watu
kama 900,000 hivi Uingereza nao watakuwa kazini kama kawaida.
Katika wafanyakazi hao, wapo 168,000
ambao ni watoaji wa huduma za afya na matibabu kama madaktari, manesi
pamoja na wauguzi ambao wanatakiwa kuwa kazini kushughulika na majukumu
yao ya kila siku.
Pia kwenye kundi la wafanyakazi hao,
wapo pia Askari Polisi 22,000 pamoja na walinzi 28,000 nao watakuwa
kazini pia kuhakikisha usalama wa siku nzima… pia wapo wapishi 42,000 na
wahudumu 28,000 wa bar ambao nao watakuwa na kibarua kuhakikisha
wanahudumia kwenye maeneo yao ya kazi.
Kwenye idadi hiyo wapo pia watu 20,000
ambao ni watumishi kwenye nyumba za ibada, nao watakuwa kwenye majukumu
yao siku hiyo… kwa hiyo kama na wewe uko kwenye majukumu siku hiyo
usisononeke, hii ni ripoti kutoka Uingereza pia.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment