Uchaguzi wa wabunge Tanga na Arusha..
Zikiwa zimebaki siku chache za kupiga kura kwenye uchaguzi wa wabunge Tanga & Arusha..,sasa hapa ninakusogezea kile kilichozungumzwa na Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kuhusiana na chaguzi hizo.
‘Taratibu
ni zile zile saa kumi jioni ikifika vituo vyote vinafungwa lakini wale
ambao wapo kwenye mistari tutahakikisha kwamba wote watapiga kura….pili
mwananchi anapoenda kupiga kura aende na kadi yaani wale
waliojiandikisha ili aweze kushiriki zoezi la kupiga kura‘>>>Lubuva
‘Hivyo kwa mawakala wajibu wao unabaki ule ule kwamba masilahi ya vyama vyao masilahi ya wagombea wao yanatekelezwa…mawakala wa vyama wa siasa wanaruhusiwa kuwepo vituoni kwa mujibu wa sheria na kanuni wakala asiyekuwa na barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi hatoruhusiwa kuingia katika chumba cha kupigia kura’>>>> Lubuva
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekcuhablog
No comments:
Post a Comment