Tangakumekuchablog
Tanga, NAIBU
Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora), Seleman Jaffo,
amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi na kuacha kupikiana majungu
na kusema kuwa yoyote ambaye hawezi
kuachia ngazi.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa
pili wa Chama Cha Wafanyakazi Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU) juzi
mjini hapa, Jaffo alisema ofisi yake haitomvumilia mtumishi ambaye hayuko
tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi.
Alisema kuna baadhi ya watumishi
wamekuwa chanzo cha kurejesha nyuma maendeleo ya wananchi na kufanya ubadhrifu
wa miradi ya maendeleo na hivyo kuagiza yoyote ambaye hayuko tayari kufanya
kazi kisheria ni vyema akaachia ngazi.
“Nitoe wito kupitia kwenu najua
salamu hizi zitawafikia kwani muko kutoka kila pembe ya taifa letu----mtumishi
yoyote wa umma ambaye hayuko tayari kufanya kazi nasi ni bora aachie ngazi”
alisema Jaffo na kuongeza
“Serikali imekuwa ikipata malalamiko
kila pembe ya ubadhirifu wa pesa za wananchi na utendaji mbovu----hili tunasema
halivumiliki na kama ni kutumbua majipu tutasaidiana kuyatumbua” alisema
Aliwataka watumishi haokila mmoja kuwajibika
na kuwatumikia wananchi ikiwa lengo ni kuleta maendeleo na kuacha kupikia na
majungu ambayo hayana nafasi kwa wananchi na Taifa.
Akizungumza katika mkutano huo,
Katibu Mkuu wa THTU, Kulu Maswanya, alimtaka Naibu Waziri, Seleman Jaffo,
kulishughulikia tatizo la watumishi kupandishwa vyeo pamoja na malipo.
Alisema kuna tatizo la muda mrefu
la watumishi kupandishwa vyeo na malipo
yao kufanyika ya zamani hivyo kumtaka kukifikisha kilio hicho kunakohusika kwa
madai kuwa limekuwa sugu.
‘Mheshimiwa Seleman tunakuomba
utufikishie kilio chetu cha kupandishwa cheo na malipo-----tumezoea kuona
watumishi wakipandishwa vyeo lakini mishaahara yao inabaki vilevile” alisema
Maswanya
Aliwataka watumishi hao kufuata
maadili ya utumishi wa uma pamoja na kutoa huduma kwa wananchi kwa uadilifu na
kuacha kuendesha shughuli kwa njia za panya.
Mwisho
Watumishi na Wafanyakazi Taasisi za Elimu za juu Tanzania (THTU) wakiimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi wakati wa kongamano lilifanyika Tanga juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Thea Ntara, akizungumza na waandishi wa habari wa Tanga mara baada ya kumalizika kongamano la Wafanyakazi Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (THTU) lilifanyika juzi.
No comments:
Post a Comment