Hizi ndio mechi 16 zitakazoamua ni timu ipi itatinga hatua ya 16 bora ya UEFA December 8 na 9 …
Hatua ya makundi ya mechi za Klabu Bingwa barani Ulaya
inamalizika leo Jumanne ya December 8 na Jumatano ya December 9 kwa
mechi 16 kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, baada ya
kupigwa michezo hii ndio tutapata picha halisi ya timu gani 16
zimefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kati ya timu 32 zinazoshiriki
michuano hiyo, licha ya kuwa kuna baadhi ya timu zimeshajithibitishia
kufuzu hatua ya 16 toka mechi zilizopita ikiwemo FC Bayern Munich. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee ratiba kamili ya mechi 16 zitakazofunga hatua ya Makundi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment