Baada ya Fabregas kuzomewa na mashabiki wa Chelsea, Pedro kaamua kuongea haya ….
December 19 Ligi Kuu Uingereza
iliendelea na moja ya mechi zilizochezwa ni ile ya Chelsea dhidi ya
Sunderland, mchezo uliomalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli
3-1. Katika mchezo huo, mashabiki wa Chelsea walionekana kumzomea
Fabregas kwa kauli yake aliyoitoa juu ya Diego Costa kuwa anachangia
kupata matokeo mabovu kwa timu hiyo.
Mshambuliaji Pedro Rodriguez
hakufurahishwa na kitendo hicho hivyo kufikia hatua ya kumpa maneno
yenye faraja kiungo Cesc Fabregas, baada ya kuzomewa na mashabiki wake
kwenye mchezo na Sunderland wakati bado anaamini bado ni mchezaji mwenye
uwezo mkubwa.
“Ulikuwa
ni wakati mgumu kwake ila ninaamini anapitia wakati mgumu, ni mchezaji
imara, mwenye uwezo mkubwa na ana sifa nzuri ndani ya klabu na ni
mshindi mpaka hapo alipo. Ninaelewa mashabiki wetu wana hasira kwa sasa,
na hii ni hali ya kawaida pindi timu na Kocha wanapokuwa katika hali
kama hii” >>>>Pedro.
Kauli ya Cesc Fabregas ilikuja siku
chache kabla ya uongozi wa klabu ya Chelsea haujamfukuza aliyekuwa kocha
wa timu hiyo Jose Mourinho. Hivyo lawama za Fabregas kwa Diego Costa
zimemfanya aingie katika matizoni kwa mashabiki kumzoea kutokana na
lawama zake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment