Wednesday, December 16, 2015

SAA ZA MOURINHO DARAJANI ZAHESABIKA



Roman Abramovich atalazimika kutoa pauni milioni 40 kumlipa Kocha Jose Mourinho kama atataka kumfukuza kazi.
Hali ya Chelsea si nzuri katika Ligi Kuu England, imekuwa zaidi ya mbaya na mhshangao ni hivi, vipi Mourinho yupo tu.
Ukweli ni kiwango cha juu cha fedha kwa kuwa Mreno huyo ana mkataba wa miaka minne na ndiyo mbichi kabisa.
Taarifa zinasema bilionea huyo wa Kirusi ameitisha mkutano wa dharura na watu wa ufundi wakiwemo wale wa bodi.
Hao ndiyo watakuwa na uamuzi wa mwisho kuwa Mourinho anayelipwa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki, abaki au aende.

Wakati anarejea Chelsea, watu hao wa bodi walipiga kura na ikawa 3-2 kuwa arejee. Kwa kipindi kilivyo sasa, inaonekana huenda ikawa 4-1, aendelee.

No comments:

Post a Comment