Salamu kutoka kwa Rais Magufuli kwa waathirika wa ajali ya December 18 Iringa..
December 18 2015 nilikusogezea ripoti kutoka Iringa Tanzania, ilihusu ajali ya basi la abiria la Kampuni ya New Force Ltd
ambalo lililongana na lori la mbao lilibeba mbao kutoka Njombe
kwenda Dar es Salaam… watu 12 walifariki na wengine zaidi ya 20
kujeruhiwa.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa wote waliofariki kwenye ajali hiyo.
Kwenye barua hiyo toka Ikulu, hii ni nukuu ya alichokisema Rais Magufuli >> ‘Nimesikitishwa
sana kutokea ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao
na ninawaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao‘- Rais John P. Magufuli.
Barua yote kutoka Ikulu ii hapa
No comments:
Post a Comment