Eti ndege zimetelekezwa na mwenyewe
hafahamiki ??!! Kichwa cha habari huenda kikakushtua lakini ndio hivyo,
na ndege zenyewe zimekaa airport mwaka mzima uwanja wa Kuala Lumpur, Malaysia.
Baada ya ndege hizo kutekelezwa uwanjani
hapo kwa zaidi ya mwaka mmoja, ilibidi uongozi wa uwanja huo wapeleke
matangazo magazetini kutaarifu kwamba kwa mmiliki wa ndege hizo
ajitokeze kutoa ndege zake ndani ya siku 14, kama asipotokea basi ndege
hizo zinauzwa !!
Baada ya tangazo hilo kutoka magazetini December 09 2015 na kuchukua headlines mitandaoni, taarifa nyingine iliyonifikia na kuripotiwa na mtandao wa Daily Mail ni kwamba Kampuni ya Swift Air Cargo imejitokeza na kusema wao ndio wamiliki wa ndege hizo tatu kubwa za mizigo…
Uongozi wa uwanja huo bado wanaendelea
na uchunguzi kujithibitishia kama kweli Swift Air Cargo ndio wamiliki
halali wa ndege hizo… lakini cha kujiuliza ni kwamba, inakuwaje mpaka
ndege zikasahaulika airiport kwa mwaka mzima ??!!
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment