Sunday, December 27, 2015

SINTOFAHAMU ZA ARSENAL, MANCHESTER NA PEP GUARDIOLA

Yalioandikwa Dec 27 kuhusu Van Gaal, Wenger na Pep Guardiola kupigiwa simu na Rais wa PSG

Kama kawaida kila linalonifikia siachi kukujuza, ninazo headlines za stori za soka za Ulaya, ninazo headlines kuhusu maendeleo ya stori za maisha ya Louis van Gaal ndani ya Man United, ninazo stori kuhusu anayetajwa kuwa kocha ghali zaidi duniani Pep Guardiola, bila kusahau headlines za mkali wa Man United Michael Carrick. Haya ndio yalioandikwa leo December 27.
Nahodha msaidizi wa Man United Michael Carrick ametoa kauli ambayo inajaribu kuweka sawa hali ya upepo ilivyo kwa sasa ndani ya Man United ambayo jana ilivunja rekodi yake ya kufungwa mara nne mfululizo rekodi ambayo kwa mara ya kwanza ilitokea mwaka 1961, kauli hiyo imekuja wakati ambao Louis van Gaal anasubiria hatma yake. “Kama wachezaji, viongozi na kocha tupo pamoja tunatakiwa tuungane na kuhakikisha tunashinda mechi, wote tunatakiwa kuwajibika kwani tupo katika kipindi kigumu na kinaumiza, kiukweli kwa sasa hatuchezi vizuri kama timu”
LVG13
Louis van Gaal
Baada ya kipigo cha Arsenal cha goli 4-0 dhidi ya Southampton usiku wa December 26, kocha wa klabu Arsenal Arsene Wenger kaongea maneno haya kuhusu staa aliyeshine usiku ule Shane Long “Najua St Mary’s ilikuwa ni sehemu ngumu kupata matokeo, tumekosa nafasi kadhaa ila Shane Long alifanya mchezo uwe mgumu zaidi , siwezi kukataa au kupuuzia kiukweli hatukucheza vizuri” 
Wenger19
Arsene Wenger
Anayetajwa kuwa kocha mwenye thamani zaidi duniani kwa sasa Pep Guardiola amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na vilabu vya Uingereza kama Man United, Chelsea na kwa kiasi kikubwa Man City, December 27 zimeandikwa stori zake na gazeti la Catalan kuhusu Rais wa PSG Nasser Al Khelaifi kumpigia simu na kuanza kumshawishi ajiunge na PSG.
Guardiola5
Pep Guardiola
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumkuchablog

No comments:

Post a Comment