Usiku wa Dec 21 Ozil kaweka rekodi hii, hakuna mchezaji yoyote wa Ligi 5 kubwa Ulaya aliyeifikia msimu huu …
Usiku wa December 21 klabu ya Arsenal inayofundishwa na kocha wa kifaransa Arsene Wenger iliingia katika headlines za ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Manchester City katika dimba la Emirates. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Oliver Giroud, ila stori kubwa haikuwa ushindi wa Arsenal.
Kwani katika mitandao ya kijamii alitawala sana kiungo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Mesut Ozil, ndio jamaa aliyotoa pasi za magoli yote mawili ya Arsenal. Ozil
kwa sasa ndio anakuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi nyingi katika
michezo michache, kwani ametoa jumla ya pasi 15 katika michezo 16 ya
Ligi Kuu msimu huu.
Kwa mujibu wa rekodi kuna jumla ya
wachezaji watano ndio wanashikilia rekodi ya muda wote ya utoaji wa pasi
nyingi za magoli katika Ligi Kuu Uingereza, miongoni mwa hao ni mkongwe
wa Arsenal Thierry Henry. Ozil ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi nyingi za magoli.
No comments:
Post a Comment