Tangakumekuchablog
Tanga, WAUMINI
wa Dini ya Kikristo wametakiwa kuwa na imni ya watoto wanaoishi katika mazingira
magumu ikiwa na pamoja na kuwapa misaada ya kielimu na kiafya na kuweza kuishi
kama wengine.
Akizungumza katika sherehe ya
Sikukuu ya Krismass jana, Mchungaji wa Kanisa la Gloryland la Sabasaba, Manase
Maganga, aliwataka wazazi na walezi kuwa na moyo wa huruma kwa watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
Alisema kuna wimbi kubwa la watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na kukimbilia mjini ambako hujishughulisha na
utumikishwaji wa kazi ngumu na baadhi kujitumbukiza katika vitendo vya uporaji
na uvutaji bangi.
“Leo tunasherehekea sikukuu ya
krismass wakubwa kwa wadogo pamoja na watoto wetu, furaha hii iwe endelevu kwa
wote hata wale wanaoishi katika mazingira magumu” alisema Maganga na kuongeza
“Kuna wimbi kubwa la watoto wa
mitaani waliokimbia masomo na wazazi wao na kukimbilia mjini, hili ni janga
hivyo kwa pamoja tushirikiane na waweze kupata haki yao ya masomo shuleni”
alisema
Maganga alisema watoto wa mitaani
wamekuwa kero kwa madai kuwa wengi wao ndio waliojitumbukiza katika vitendo vya
uporaji na ubwiaji wa unga na hivyo
kutaka ushirikiano wa wazazi na walezi ili kumaliza tatizo hilo.
Kwa upande wake mzee wa kanisa hilo,
Saimon Molely, alisema kanisa hilo kila mwaka limekuwa na da ya kutoa sadaka
kwa wazee na watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Alisema katika sherehe hiyo
wamewasaidia wazee na vijana walioathirika na madawa ya kulevya kwa kuwata
Televisheni ili kituoni kwao waweze kujifunza na kujua ubaya wa madawa ya
kulevya.
“Tumetoa mashuka nguo na televisheni
kwa waathirika wa madawa ya kulevya wanaoishi katika nyumba maalumu , hii ni
kuwa siku ya leo ni furaha kwa watu wote” alisema Molely.
Molely alisema kanisa litaendelea
kutoa misaada kwa watu mbalimbali wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo
wazee na vyakati za majanga hivyo kuwataka waumini wa dini hiyo kuwaombea
viongozi wao uzima na afya njema ili kuwatumikia.
Mwisho
Waumini wa Kanisa la Gloryland
Sabasaba Tanga, wakiliombea Taifa amani na kumtakia afya njema Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kutekeleza majukumu yake pamoja na
kupiga vita Umasikini na Ufisadi wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Krismass jana.
Kiongozi wa Waathirika wa Madawa ya Kulevya (Soba House) Tanga, Hamza Mkanga, akipokea Televisheni moja, king’amuzi na chupa ya chai kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa la Gloryland la Sabasaba Tanga, Manase Maganga, ikiwa ni zawadi ya Krismass
No comments:
Post a Comment