RIP mtu mnene kuliko wote duniani, kutana na picha za mwili wake wakati wa uhai wake
Unakumbuka au umwahi kusikia zile
headlines za mtu mnene kuliko wote duniani, basi imenifikia stori yake
mpya japokuwa sio njema ,. Andres Moreno jamaa ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mtu mnene duniani amefariki dunia December 25 siku ya sikukuu ya Chrismass.
Stori kutoka indianexpress.com zinaeleza Andres Moreno ambaye
alikuwa anatajwa kuwa na uzito wa Kilogram 450 ameaga dunia asubuhi ya
December 25 siku ya Chrismass kwa tatizo la moyo, tatizo ambalo
limetokana na kuwa mnene kupita kiasi. Andres Moreno amefariki akiwa na umri wa miaka 38.
Licha ya jitihada za kuokoa maisha yake kufanyika kwa kuchukuliwa na Ambulace kutoka nyumbani kwake Sonora Mexico na kuwahishwa St Jose Hospital,
lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda. Ripoti ya madaktari imesema
December 26 kuhusu tatizo lililopelekea kuchukua uhai wake.
No comments:
Post a Comment