Kauli ya Wayne Rooney kuhusu ajira ya Louis van Gaal na walichoamua wachezaji wa Man United …
Bado hali sio nzuri ndani ya klabu ya Man United, haikatishi siku bila mitandao ya kijamii, magazeti na tovuti kujadili juu ya kibarua cha kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal,
mengi yameandikwa na kwakuwa Uingereza ndio Ligi inayopendwa na vyombo
vya habari vya nchi hiyo vina nguvu, basi usishangae kuona nakuletea
stori nyingine kutoka Man United.
December 24 nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney amefunguka kuhusu wachezaji wenzake wanavyowaza namna ya kupambana na kuokoa kibarua cha kocha wao Louis van Gaal ambaye anatajwa kuwa katika wakati mgumu, na kama timu yake ikifanya vibaya katika mchezo dhidi ya Stoke City ndio atakuwa katika wakati mgumu zaidi.
“Kiukweli
kuna watu wengi ambao wanazungumza na kuandika vitu ambavyo havipo au
wanaamini vinaweza kutokea, watu wanaandika vitu ambavyo kiukweli
hawavijui. Kwa sasa tunajitahidi na tunapambana kubadilisha mambo
yalivyo kwa ajili ya kocha wetu, ni muhimu kuungana kwa pamoja”
>>> Wayne Rooney
Stori zinazodaiwa zilitoka kwa baadhi ya wachezji wa Man United zilinukuliwa kuwa, wachezaji hawana mahusiano mazuri na kocha Louis van Gaal katika vyumba vya kubadilishia nguo sambamba na wachezaji kukosa mzuka wa kucheza, maneno ambayo kwa mujibu wa kauli ya Rooney, inaashiria kuwa sio kweli ni mambo yanayoandikwa.
Kwa habari,matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment