Kinachofatia ni hiki kwenye Chuo kilichofungwa Kenya baada ya shambulio la kigaidi..
Kuna vyuo vina majina makubwa Kenya kama Nairobi University, Kenya University.. jina la Garissa University lilifahamika na kusikika zaidi baada ya kutokea shambulio la kigaidi na kupelekea mauaji ya wanafunzi zaidi ya 140.
Ripoti nyingine kutoka Kenya
imethibitisha kwamba Kikao kitakachofanyika ndani ya wiki mbili kuanzia
leo kitaamua lini Chuo hicho kitafunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi
nane.
Makamu wa Rais Kenya, William Ruto
ameonana na baadhi ya viongozi wa eneo la Garissa, kaskazini mwa Kenya
na kuwahakikishia kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha
hali ya usalama inakuwa sawa kwenye maeneo hayo ambayo yamekuwa
yakikumbwa na mashambulizi ya kigaidi mara nyingi.
Tukio la shambulio hilo ni moja ya matukio ambao yaliwaumiza sana Wakenya kwenye mwaka 2015.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment