Monday, December 28, 2015

MAAJABU NA KWELI

mzee aliyesafiri kwa miezi saba pekeyake baharini kutoka Marekani..

Kwenye vitu ama stori ambazo zimeonekana kukamata vichwa vya habari vya kimataifa kwa saa kadhaa mfululizo pamoja na mitandao mikubwa, iko pia stori ya mzee mwenye umri wa miaka 53, jina lake ni John Beeden.
Mzee Joe alianza safari yake San Francisco Marekani siku ya June 1 2015 akiwa na boti yake ndogondogo na kufanikiwa kufika Jiji la Cairns Australia, siku ya jana December 27 2015… safari yake imekamilika kwa kusafiri jumla ya siku 209 ambazo kwa hesabu nyingine ni miezi saba kamili !!
Kwa umbali ambao mzee huyo amesafiri, hesabu zinaonesha kuwa amekuwa akisafiri kwa jumla ya saa 15 kila siku ambapo ina maana kwa siku alikuwa na saa kama tisa tu za kupumzika.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment