Saturday, December 19, 2015

MAKONDE YARINDIKA UCHAGUZI WA MEYA JIJI LA TANGA





 Diwani kata ya Chumbageni halmashauri ya jiji la Tanga, Saida Gaddafi (CCM) akipiga kura kumchagua Meya wa jiji la Tanga uchaguzi uliofanyika leo   ambapo ulikuwa na wagombea wawili, Rashid Jumbe wa CUF na Suleiman Mustapha maarufu kama Sele Boss.




 Diwani kata ya Mwanzange Rashid Jumbe (CUF) ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya Umeya wa jiji la Tanga akipiga kura kumpata Meya wa jiji hilo uliokuwa na wagombea wawili CCM na CUF.


Diwani kata ya Ngamiani kati, Habibu Mpa (CUF) akipiga kura kumchagua Meya halmashauri ya jiji la Tanga  leo nafasi ambayo ilikuwa ikigombewa na wagombea wawili, Rashid Jumbe (CUF) na Suleiman Mustapha (CCM).
 Diwani wa Chama Cha Wananchi (CUF) akibishana na Askari wa usalama kupinga matokeo yaliyompa Umeya  na Mgombea wa CCM , Suleiman Mustaffa kuibuka mshindi dhidi ya Rashid Jumbe wa CUF.

 Madiwani wa CCM na CUF wakichapana makonde kupinga ushindi wa mgombea nafasi ya Umeya , Suleiman Mustaffa (CCM)  baada ya Mkurugenzi wa jiji, Daudi Mayegi kumtangaza Mshindi wa nafasi hiyo.


  Askari wa kikosi cha FFU wakiwazuia Madiwani wa CUF wakiongozwa na Mbunge wa Mussa Mbarouk (CUF) waliotaka kuingia ofisi ya Mkurugenzi yalikohifadhiwa masanduku ya kura kwa madai yahesabiwe tena kupinga ushindi wa mgombea wa nafasi ya Umeya, Suleiman Mustaffa maarufu kama Sele Boss.

No comments:

Post a Comment