Monday, December 7, 2015

KASI YA MAGUFULI NI MWENDO MDUNDO

Wengine wamesimamishwa leo..

Mpaka leo hii December 07 2015 tunahesabu kama mwezi mmoja hivi umepita tangu Rais Magufuli aapishwe na aanze kazi ya Urais wa awamu ya tano Tanzania.
Mfululizo wa stori zenye uzito wa kasi yake kwenye Urais zimekuwa zikitufikia kila siku, ya leo bado inabeba headlines za bandarini kwa mara nyingine… tangu siku ya kwanza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amefanya ziara ya ghafla bandarini mengi yameripotiwa ikiwemo ishu ya ubadhirifu, rushwa, kukwepa kodi ya upotevu wa makontena.
Mpya iliyonifikia kutoka bandarini inahusu kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa bandari, Awadhi Massawe, na pia kuvunja bodi ya bandari Dar es Salaam.
Kingine ni kwamba Rais Magufuli pia amemsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shabani Mwanjaka.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment