Sunday, December 20, 2015

HOFU YA BOMU YAILAZIMISHA NDEGE YA UFARANSA KUTUA KENYA

Hofu ya bomu ilivyolazimisha ndege ya Ufaransa kutua Kenya kwa dharura.

Ndege ya abiria ya Air France Boeing 777 AF463 iliyokuwa ikifanya safari yake kati ya Mauritius na Paris ililazimika kutua ghafla katika uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya baada ya kuwepo hofu ya bomu ndani ya ndege hiyo.
Wakati iko angani kuna kitu kilichodhaniwa kuwa bomu kilipatikana ndani ya choo cha ndege hiyo na muhudumu mmoja akachukua hatua ya kumfahamisha Rubani kuhusiana na hicho kifaa ndipo shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
AirFRANCE
AirFRANCE 2
Katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kamanda mkuu wa polisi Kenya Jenerali Joseph Boinnet, amesema kuwa ndege hiyo iliyokuwa njiani kuelekea Paris Ufaransa ikiwa na abiria 473 na wahudumu 14 na ilitua salama na abiria wote kuokolewa.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment