Ni kweli Pep Guardiola kaamua hivi kuhusu Man City? Ujerumani wameandika hivi …
Kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola
jina lake limekuwa likitumika kupamba headlines tofauti tofauti za
magazeti ya michezo barani Ulaya na Afrika, hususani juu ya stori za
kocha huyo kuhusishwa kutaka kujiunga na Man City ila Chelsea na Man United wanahusishwa kunyemelea huduma ya kocha huyo pia.
Guardiola ambaye kwa sasa ndio anatajwa kuwa kocha ghali, ameandikwa na gazeti la Ujerumani kuwa tayari ameasaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Man City, mkataba ambao unatajwa kuwa na thamani ya euro milioni 25 kwa mwaka. Stori kutoka gazeti la Kijerumani la Bild, inapewa nafasi kubwa ya kuaminika kutokana na moja kati ya viongozi wa FC Bayern alikiri kuwa Guardiola anaondoka na tayri kasema klabu anayotaka kwenda.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment