Watuhumiwa wa kesi ya makontena 349 bandarini walivyofikishwa Mahakamani Dar jana.
Kama ulipitwa na hii stori iliripotiwa kwenye habari ya kituo cha ITV jana kuhusu ishu ya kufikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa kutoka Mamlaka ya TRA ambao walisimamishwa kazi kutokana na kuhusishwa na tuhuma za upotevu wa makontena 349 bandarini Dar.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipita bandarini siku ya Ijumaa November 27 2015
na kukutana na hiyo ishu ya makontena hayo kupotea na pia kubaini
kuwepo kwa ubadhirifu ambao umepelekea Serikali ya Tanzania kukosa
mapato kupitia kodi… Jeshi la Polisi likapewa jukumu la kuwakamata
watumishi hao 12 na kuendelea na taratibu nyingine za kuwawajibisha.
Jana watuhumiwa nane kati wa kesi hiyo wamefikishwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashtaka ya kesi zao, baadae kesi ikaahirishwa mpaka December 17 2015 ambapo Mahakama hiyo ilikataa kuwapa dhamana watuhumiwa wote.
Hapa ninazo picha kutoka Blog ya Issa Michuzi ilivyokuwa Mahakama ya Kisutu jana.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment