Kilichojiri Old Trafford kati ya Man United Vs Chelsea, kutana na matokeo ya mechi za EPL
Michezo 8 ya Ligi Kuu Uingereza imechezwa jana Jumatatu ya December 28, ikiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Uingereza, mechi ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa na hisia za mashabiki wengi wa soka, ni mchezo kati ya Man United dhidi ya klabu ya Chelsea iliyomtimua Jose Mourinho hivi karibuni na kumpa kibarua cha muda Guus Hiddink.
Mvuto wa mchezo huu unakuja kufuatia vilabu hivyo viwili kutofanya vizuri kiasi hata, Chelsea kufikia maamuzi ya kumfuta kazi Jose Mourinho, wakati Man United wakiwa wanahusishwa kuwa katika mpango kama huo wa kutaka kumfukuza kocha wake wa kiholanzi Louis van Gaal.
Mchezo huo ambao ulikuwa umeteka hisia za watu wengi umemamlizika kwa sare ya kutofunga, kwa matokeo hayo Man United wanakuwa nafasi ya 6 ikiwa na point 30, wakati klabu ya Chelsea itakuwa nafasi ya 14 baada ya sare hiyo na kufanya itimize jumla ya point 20.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa December 28
- Crystal Palace 0-0 Swansea
- Everton 3-4 Stoke
- Norwich 2-0 Aston Villa
- Watford 1-2 Tottenham
- West Brom 1-0 Newcastle
- Arsenal 2-0 Bournemouth
- Man Utd 0-0 Chelsea
- West Ham 2-1 Southampton
No comments:
Post a Comment