Tuesday, December 29, 2015

ASAJILIWA PAPO HAPO MKATABA WAVUNJWA

FC Barcelona yavunja mkataba na mchezaji saa chache baada ya kumsajili, kisa Real Madrid …

Mapenzi ya wachezaji katika vilabu fulani barani Ulaya, imekuwa kawaida hata kama hawavichezei. December 28 klabu ya FC Barcelona imeingia kwenye headlines baada ya kumsainisha mchezaji na kisha kufuta mkataba wake masaa machache baada ya kugundua kuwa ametweet vitu ambavyo vinaihusu timu ya Real Madrid.
Baada ya kufuzu majaribio na Barcelona B Sergi Guardiola alisaini mkataba lakini ulifutwa mapema, baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya jitihada za kufuatilia mtandao wake wa twitter na kuona posts ambazo zinaonesha mapenzi na Real Madrid

No comments:

Post a Comment