Louis van Gaal anaondoka Man United? imenifikia list ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi yake …
Headlines za makocha mbalimbali wa Ligi
Kuu Uingereza kufukuzwa zinaendelea kushika kasi ambapo hivi karibuni
ulimwengu ulishuhudia Kocha wa Swansea City Garry Monk akifukuzwa na Jose Mourinho akifukuzwa kuifundisha Chelsea.
Stori za mitandaoni za hivi karibuni ni zile zinazomzungumzia Kocha wa Manchester United Louis van Gaal
na hatma yake ndani ya klabu hiyo baada ya timu yake kuendelea kufanya
vibaya, hivyo kumekuwa na list ya makocha wengine wanaotajwa kurithi
nafasi yake mtu wangu.
Kupitia mtandao wa ‘The Telegraph’ pamoja na taarifa zilizopo ndani ya Manchester United zinatajwa, Kocha aliyefukuzwa kuifundisha Chelsea, Jose Mourinho yupo kwenye list ya makocha wanaotajwa kumrithi Van Gaal Man United. Mourinho alifukuzwa na Chelsea baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbovu.
Kocha mwingine anayetajwa ni Pep Guardiola ambaye anaifundisha klabu ya Bayern Munich inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani, kwani hivi karibuni alikataa kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha FC Bayern Munich. Mkataba wa Gurdiola ndani ya Bayern unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment