Hii ndio adhabu ya FIFA kwa Sepp Blatter na Michel Platini baada ya uchunguzi kufanyika
Baada ya uchnguzi wa kina kufanyika na wachunguzi wa shirikisho la soka ulimwenduni FIFA wameamua kutoa adhabu ya kuwafungia miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka aliyekuwa Rais wa soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter na Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini.
Blatter na Platini wamekumbana na adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kufanya matumizi ya fedha kinyume na taratibu. Blatter anatuhumiwa kufanya malipo ya milioni 2 za Uswiss mwaka 2011 kwenda kwa Platini kama Rais wa FIFA malipo ambayo ni kinyume na taratibu na ameshindwa kuthibitisha zilitumika kufanyia nini.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 amefungiwa miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka sambamba na faini ya 50,000 za Uswiss kutokana na kushindwa kuheshimu sheria za FIFA, wakati Platini amepigwa faini ya 80000 za Uswiss kutokana na kuhusika katika mchakato huo.
“Samahani
yangu binafsi kwa FIFA na kwa mchezo wa mpira wa miguu, nitapambana kwa
ajili yangu na FIFA, nafungiwa miaka nane kwa kosa lipi? Nitakutana na
mwanasheria wangu kujadili kipi sahihi na kipi sio sahihi na kipi ni
haki. Tutakata rufaa tena” >>> Blatter
No comments:
Post a Comment