Thursday, December 31, 2015

JESHI LA POLISI LATOA KAULI KUINGIA MWAKA MPYA

Saa chache kabla ya kufunga mwaka kuna hii taarifa kutoka Jeshi la Polisi..


Tukiwa tumebakiza masaa machache kabla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, Jeshi la Polisi limetoa tahadhari kuelekea mkesha wa mwaka mpya.
Katika taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na msemaji Advera Bulimba imesema wamejipanga vyema kukabiliana na vitendo vya uhalifu vitakavyojitokeza na kuimarisha ulinzi katika fukwe za bahari na maeneo mbalimbali ya starehe.
Taarifa hiyo pia imewataka watumia barabara kuwa makini na wananchi waache tabia ya kuchoma matairi barabarani pamoja na kupiga fataki kwani hatua hali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi..
JES 1 JES 2

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment