Wednesday, December 9, 2015

MGOGORO WA RELL ASET MAGAONI WAINGIA SURA MPYA



Tangakumekuchablog
Tanga, MBUNGE wa jimbo la Tanga mjini , Mussa Mbarouk  (CUF), ameitaka halmashauri ya jiji la Tanga kuumaliza mgogoro wa ardhi wa Magaoni kupisha mradi wa Rell Assert kuelekea Bandari mpya ya Mwambani.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi ulioitishwa na wahanga wa mgogoro huo jana,  wanaodai kupunjwa fidia zao , Mbarouk aliwataka wananchi hao kufika ofisi za mkurugenzi na vielelezo vyao ili  ufumbuzi  kufikia tamati.
Alisema mgogoro huo wa madai umekuwa ukiwaumiza wananchi na kuacha kufanya kazi za kujiletea maendeleo na badala yake wamekuwa wakiitisha vikao visivyokuwa na mwisho.
“Mgogoro huu ni wa muda mrefu na umekuwa ukiwaumiza na kushindwa kujua hatma ya majengo na viwanja vyenu----ili kumalizwa niiombe halmashauri kukaa na wahanga hawa ili kufikia tamati” alisema na kuongeza
“Kama fidia ilifanyika mbona kuna malalamiko ya watu kudai kupunjwa na wengine kukosa kabisa----hatutaki malalamiko tunachotaka ni maendeleo” alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mgogoro wa Rell Asset, Hamad Salim Chembea, amesema awali wakati uthamini wa majengo na viwanja ulipofannywa amedai makubaliano siyo yaliyofanyika.
Alisema malipo yaliyofanyika hayaendani na makubaliano hivyo kuitaka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makaazi kuingilia kati vyenginevyo kunaweza kutokea mgogoro mkubwa wa kisheria.
“Tunaiomba halmashauri ya jiji kuingilia kati kupata malipo yetu kwa haki----tumefukuzwa bila kupewa viwanja wala pesa kwa wengine sasa huku ni unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za binadamu” alisema Chembea
Alisema toka wahamishwe katika makazi yao wamekuwa wakiishi katika majumba ya kupanga na wengine kwa jamaa zao na kusubiri malipo na fidia ya viwanja ambapo wamekata tama.
                                                          Mwisho



 Wahanga wa mgogoro wa nyumba na viwanja Magaoni Tanga wakiwasikiliza viongozi wao kulalamikia fidia ya viwanja na nyumba kupisha mradi wa Rell Asset  kuelekea bandari mpya ya Mwambani.
  Mwenyekiti wa mgogoro wa viwanja na nyumba Magaoni Tanga,  Hamad Chembea akiwasomea baadhi ya nyaraka za makubaliano ya malipo ya nyumba na viwanja kupisha mradi wa Rell Asset jana wakati wa mkutano ulioitishwa jana.

 Mmoja wa wahanga wa mgogoro wa mashamba na viwanja Magaoni Tanga, Agrey Jofreys, akilalamika mgogoro wao kuchukua muda mrefu wa mradi wa Rell Asset na kuitaka halmashauri kutuma wathamini upya wa mashamba na nyumba.

No comments:

Post a Comment