Ndege ya abiria ilivyokatiza safari yake angani kisa Panya..
Ndege ya Air India ambayo ilikua ikitoka Mumbai kuelekea London, Uingereza ililazimika kugeuza safari ikiwa na abiria wake 171 na kurudi ilipotoka baada ya abiria kubaini kuwepo kwa panya ndani ya ndege hiyo.
Ingawa juhudi za kumpata panya huyo ziligonga mwamba lakini rubani alilazimika kurudi Mumbai ili kuwatoa wasiwasi abiria zaidi ya 170 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ndege hiyo ya shirika la ndege la India.
Baada ya kutua abiria walilazimika kubadilishiwa ndege na kuanza safari upya ya kuelea London.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment