Thursday, December 24, 2015

TAMU CHUNGU

Saa chache zimebaki kusherehekea christmas lakini kwingine imepigwa marufuku!!

Najua wakristo wengi duniani wanahesabu saa chache kuifikia December 25, siku ambayo inasherehekewa sikukuu ya Christmas kila mwaka… kama na wewe umejiandaa vizuri na sherehe hiyo basi nikutakie heri mtu wangu, lakini stori ina kichwa cha habari tofauti kutoka Somalia.
Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za christmas kwa siku ya kesho, moja ya sababu iliyotajwa ni kwamba sherehe hizo zitasababisha hofu kwa watu wa dini nyingine ambao hawahusiani nazo.
Wageni toka nchi nyingine wameruhusiwa kufanya sherehe zao majumbani mwao, lakini maeneo kama mahotelini na maeneo mengine yamezuiwa kufanyika sherehe zozote kwa siku ya kesho huku Serikali ikiimarisha ulinzi kuhakikisha agizo hilo linazingatiwa.

No comments:

Post a Comment