Friday, December 4, 2015

FLOYD MAYWEATHER NA MAPESA YAKE

Zawadi za krismasi zimeanza kumfikia Floyd Mayweather hii imetoka kwa mashabiki wake

Siku zote unapoambiwa utaje list ya mastaa waliowahi kutamba katika mchezo wa ngumi, hauwezi ukaliacha jina la Floyd Mayweather mtu wangu. Staa huyo ambaye ni bingwa wa mchezo wa ngumi wa uzito wa kati amepokea zawadi ya Tiger mwenye miezi miwili toka kwa mashabiki wake kwa ajili ya Krismasi.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mayweather alipost picha akiwa na Tiger huyo, ambapo kwenye caption ya picha hiyo, aliandika kuwashukuru mashabiki wake wa jiji la Moscow Urusi, kwa zawadi ya Krismas waliyompatia pamoja na kuwaomba wamchagulie jina la Tiger huyo.
2F09F84F00000578-0-image-a-34_1449188627737
“Napenda kuishukuru familia yangu pamoja na mashabiki wangu toka Moscow kwa upendo waliouonyesha wa kunizawadia Tiger kwa ajili ya Krismasi, ni kitu kigeni toka kwangu, jina gani nimpatie Tiger huyu wa kike mwenye miezi miwili?”>>>Mayweather.
2F0C912200000578-3345339-Mayweather_s_personal_assistant_Marikit_Laurico_is_pictured_stro-a-3_1449217993499
Msaidizi wa Mayweather ambaye anaitwa Marikit Laurico akipiga picha na Tiger wa miezi miwili aliyopewa zawadi Mayweather.
Floyd Mayweather ambaye hivi karibuni alitangaza kustaafu mchezo wa ngumi baada ya kupigana pambano lake la mwisho na bondia Andre Berto na kumpiga, pambano ambalo lilimfanya Floyd Mayweather kupambana jumla ya mapambano 49 na kuendeleza rekodi yake ya kushinda mapambano yote.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment