Ripoti kutoka Zanzibar kuhusu ajali ya moto kwenye meli December 15..
Hii stori imenifikia baada ya kuenea kwenye mitandao pamoja na picha zikionesha tukio la meli kuwaka moto
Nimeipata ripoti pia kwenye habari ya ITV kwamba meli hiyo ya MV Royal
imepata ajali ya kuwaka moto ikiwa katikati ya safari kutoka Unguja
kwenda Pemba, moto huo umeunguza injini za meli hiyo lakini kwa bahati
nzuri ikatokea meli nyingine ya MV Serengeti, ambapo ikafanyika kazi ya kuokoa abiria waliokuwa kwenye meli hiyo pamoja na kuuzima moto huo.
Kamanda wa Polisi Pemba, Shehan Mohamed Shehan amesema
meli ilikuwa na abiria zaidi ya 300 pamoja na watoto 70.. wote wametoka
salama na meli imefanikiwa kuvutwa mpaka bandarini Pemba.
No comments:
Post a Comment