Makumi ya maelfu ya
watu wanatarajiwa kumuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali
nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.
Bingwa huyo wa ndondi katika uzani mzito duniani na mwanaharakati alifariki siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74. Umati mkubwa wa watu utachukua mwili wake na kuupitisha katika maeneo muhimu ya maisha yake kabla ya kuufanyia ibada.
Muingizaji
Will Smith na aliyekuwa bondia Lenox Lewis watakuwa miongoni mwa wale
watakaobeba jeneza lake ,huku aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton
akitarajiwa kutoa hotuba. Msafara wa jeneza lake ulianza saa tatu saa za
Marekani na kulipitisha jeneza hilo nyumbani kwake,katika kituo cha
Ali,baadaye kupitishwa katika kituo cha makavazi ya watu weusi nchini
Marekani na baadaye katika eneo la Muhammad Ali Boulevard. Miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ni rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan na mfamle Abdullah wa Jordan.
Rais
Obama hatakuwepo,kwa kuwa anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kufuzu kwa
mahafala ya mwanawe mkubwa Malia.Mshauri mkuu wa ikulu ya rais Valerie
Jarret ambaye alimjua Ali atamwakilisha rais. Lennox Lewis aliyekuwa bondia wa uzani mkubwa dunia
kabla ya kustaafu kwake amesema kuwa ni heshimu kubwa kwake kuorodheshwa
miongoni mwa wale watakaobeba jeneza la marehemu huku akisema kuwa
kumbukumbu za Ali hazitasaulika. Ali alitaka ibada ya Janazah kuwa wakati wa mafunzo kulingana na Imam zaid Shakir alieongoza ibada hiyo.
Msomi
wa Kiislamu Sherman Jackson alisema:Kufariki kwa Muhammad Ali
kumetufanya tujisikie wapweke duniani.''Kitu kizima,kitu kikubwa na
kinachovutia na kinachotoa uhakika wa maisha kimetuwacha''.
Baada ya kujiuzulu,uvumi ulianza kuhusu hali yake ya
kiafya.Ugonjwa wa kutetetemeka mwili baadaye ulipatikana lakini Ali
aliendelea kuwepo katika maeneo ya hadhara huku akipokewa vizuri kila
anapoenda.
BBC
No comments:
Post a Comment