Chemba iliyoko mtaa wa Lumumba barabara ya 13 kwa 14 Ngamiani Tanga ikitiririsha maji machafu barabarani na kuwa kero kwa wakati wa eneo hilo na wapita njia jambo ambalo baadhi ya wakazi wameiambia kuwa kipindupindu kinawanyemelea.
Chemba hiyo ambayo inatoa harufu kali na kuwapa shida wakazi hao wamedai kuwa hata nyakati za kula na kunywa wanapata shida baada ya harufu yote kuwaingia kinywani.
Tangakumekuchablog imeshuhudia wakazi wa eneo hilo na watumaiji wa barabara hiyo wanavyopata shida ya kupita na kufanya shughuili zao za kila siku
No comments:
Post a Comment