Euro2016: Leo mechi tatu zachezwa

Leo kuna mechi
tatu katika kinyanganyiro cha mataifa bingwa barani Ulaya. Mechi ya
kwanza ni ya kundi la D kati ya Uturuki na Croatia ambayo itachezwa
mjini Paris.
Katika kundi la C, Ireland Kaskazini ambayo ilifuzu
kwa kombe hilo kwa mara ya kwanza kabisa, watacheza mechi yao ya
ufunguzi dhidi ya Poland katika mji wa Nice.Ujerumani walioshinda kombe hilo mara ya mwisho miaka 20 iliyopita, itapambana na Ukrain karibu na mji wa Lille.
No comments:
Post a Comment