Virusi sawa na HIV ya paka vyagunduliwa Kenya
Nchini
Kenya, virusi hatari aina ya FIV, vinaavyofananana kabisa na virusi vya
HIV vinavyosababisha Ukimwi vimegunduliwa katika paka mmoja kupitia
uchunguzi wa kimaabara.Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wameonywa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua.
Madaktari wa maabara ya Lancet mjini Nairobi Waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani.
Hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowowte wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
BBC
No comments:
Post a Comment